MEXICO-CORONA-AFYA

Coronavirus: Mexico yakaribia kufikisha visa 300,000 vya maambukizi

Mexico sasa ni nchi ya nne kwa kuathirika zaidi na ugonjwa huo hatar wa Covid-19 duniani.
Mexico sasa ni nchi ya nne kwa kuathirika zaidi na ugonjwa huo hatar wa Covid-19 duniani. REUTERS/Gustavo Graf

Mexico imerekodi visa vipya 4,482 vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo vipya 276, Wizara ya Afya imebaini, na kusema kuwa idadi hiyo imefanya jumla ya visa vya maambukizi kufikia 299,750 na vifo 35,006.

Matangazo ya kibiashara

Serikali imesema hapo zamani kwamba idadi halisi ya watu walioambukizwa virusi vya ugonjwa huo inaweza kuwa kubwa zaidi kuliko visa vilivyothibitishwa.

Mexico sasa ni nchi ya nne kwa kuathirika zaidi na ugonjwa huo hatari wa Covid-19 duniani.

Hayo yanajiri wakati idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Brazil inakaribia milioni mbili. Hadi kufikia sasa nchi hii ina jumla ya visa zaidi ya Milioni moja kwa mujibu wa takwimu za chuo kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani.

Maambukizi ya virusi vya Corona duniani yanaendelea kuongezeka wakati huu jimbo la Florida nchini Marekani limeripoti maambukizi mapya Elfu 15 kwa muda wa saa 24 zilizopita, wakati huu serikali ya rais Donald Trump ikitaka shule kufunguliwa.

Ongezeko hili la maambukizi katika jimbo la Floroda, linalifanya kuingia kwenye vitabu vya historia vya kuripoti idadi kubwa ya maambukizi kwa siku moja hata zaidi ya taifa lolote la bara Ulaya, ambalo maambukizi hayo yameanza kupungua.

Jimbo hilo limevunja rekodi ya jimbo la New York ambalo liliwahi kuripoti visa zaidi ya Elfu 12, tarehe 10 mwezi Aprili.

Hii inaifanya Marekani kuendelea kuongoza kwa maambukizi ya virusi vya Corona, ikiwa na visa zaidi ya Milioni tatu na kufuatwa na Brazil, huku India ikiwa katika nafasi ya tatu.