MAREKANI-VENEZUELA-HAKI-USHIRIKIANO

Marekani yataka mkuu wa Mahakama Kuu ya Venezuela akamatwe

Mkuu wa Mahakama Kuu nchini Venezuela Maikel Moreno, atafutwa kwa udi na uvumba na Marekani.
Mkuu wa Mahakama Kuu nchini Venezuela Maikel Moreno, atafutwa kwa udi na uvumba na Marekani. REUTERS

Marekani imechukuwa vikwazo dhidi ya mkuu wa Mahakama Kuu ya Venezuela Maikel Moreno na kutangaza fidia ya dola milioni 5 kwa taarifa yoyote itakayohusiana na kukamatwa kwake au kushtakiwa kwa madai ya kuhusika kwake katika uhalifu wa kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa, Wizara ya Mashauriano ya Kigeni ya Marekani imesema kuwa vikwazo dhidi ya Maikel Moreno, mshirika wa Rais Nicolas Maduro ambaye Washington inafutilia mbali uhalali wake kama rais wa Venezuela, vinamzuia yeye na mkewe - kusafiri kwenda nchini Marekani.

Hivi karibuni Moreno alisema mfumo wa mahakama wa Venezuela hautakubali uwe chini ya "udhamini" wa serikali ya kigeni, na kulaani katika taarifa kwamba "mashambulizi ya kijinga, kutoka utawala wa Amerika ya Kaskazini yamejaa uzushi na uwongo" mtupu.

Mwezi Machi mwaka huu, mamlaka nchini Marekani ilimshtumu Maikel Moreno kwa makosa yanayohusiana na utakatishaji wa fedha haramu, kando ya mashtaka dhidi ya Nicolas Maduro kwa "biashara ya ugaidi".