MAREKANI-TRUMP-USALAMA-SIASA

Rais Donald Trump aongeza idadi ya maafisa wa polisi Chicago ili kupunguza uhalifu

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kutumwa kwa vikosi vya usalama katika miji ambayo hivi karibuni imeshuhudia machafuko wakati wa maandamano ya kulaani vitendo vya ubaguzi wa rangi nchini humo.

Rais aw Marekani mara kadhaa alitishi kutuma jeshi kukabiliana na waandamanaji katika miji mbalimbali nchini Marekani.
Rais aw Marekani mara kadhaa alitishi kutuma jeshi kukabiliana na waandamanaji katika miji mbalimbali nchini Marekani. REUTERS/Tom Brenner
Matangazo ya kibiashara

Miji mingi itakayoshuhudia kupelekwa kwa maafisa wa usalama inaongozwa na chama cha Democratic kama Chicago, New York, Philadelphia na Minneapolis.

Trump amesema hana budi kutuma maafisa hao wa usalama kuwalinda raia.

Hatua hii hata hivyo, imelaaniwa vikali na wanasiasa wa chama cha Democartic kwa kile alichosema, rais Trump anachukua uamuzi huo kupata umaarufu wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Novemba.

Trump amewashtumu Mameya wa miji inayoongozwa na chama cha Democratic kwa kuwaogopa waandamanaji anaowashtumu kufuja na kuharibu mali ya watu kwa sababu za kisiasa.

Mji wa Portland umekuwa ukishuhudia maandamano dhidi ya ukatili unaotekelezwa na polisi mjini humo tangu kutokea kwa mauaji ya George Floyd, Mmarekani mweusi aliyeuawa akiwa mikononi mwa polisi huko Minnesota mnamo mwezi Mei mwaka huu.

Maafisa 150 wanatarajiwa kutumwa Chicago wiki hii, ili kusaidia maafisa wengine wa serikali pamoja na maafisa polisi wa Chicago kupambana na uhalifu.