MAREKANI-CORONA-AFYA-SIASA

Trump asitisha kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa chama cha Republican kutokakana na Corona

Rais wa Marekani Donald Trump amesitisha kufanyika kwa mkutano Mkuu wa chama cha Republican, uliokuwa umepangwa kufanyika baadaye mwezi ujao katika jimbo la Florida.

Rais wa Marekani Donald Trump.
Rais wa Marekani Donald Trump. SAUL LOEB / AFP
Matangazo ya kibiashara

Trump amesema amechukua uamuzi huu kwa sababu ya kuendelea kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya Corona nchini humo, na sasa mkutano huo mkuu utakaomwidhinisha kuwa mgombea utafanyika kwa njia nyingine.

Trump anatarajiwa kupambana na aliyekuwa Makamu wa rais Joe Biden kutoka chama cha Democratic wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Novemba.

Wiki hii rais Donald Trump aliwataka Wamarekani kuvalia barakoa muda wote wanapokuwa katika maeneo ya umma, akisema kuwa ni ishara ya "uzalendo", jambo ambalo amesema yeye pia ameanza kufanya.

Marekani sasa inaripoti visa Milioni 4.11 baada ya visa vipya 70,719 kuthibitishwa.

Wagonjwa Milioni 1.23 wamepona ugonjwa huo hatari. Marekani imeripoti vifo 146, baada ya vifo vipya 1,082 kuthibitishwa.