BRAZILI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya vifo nchini Brazili yapindukia zaidi ya 85,000

Brazil inaendelea kuathirika zaidi na janga la Corona.
Brazil inaendelea kuathirika zaidi na janga la Corona. REUTERS

Brazil imerekodi kesi mpya 55,891 za maambukizi zilizothibitishwa za virusi vya ugonjwa wa Covi-19 na vifo 1,156 vipya vilivyohusishwa na janga hilo katika saa ishirini na nne zilizopita, wizara ya afya nchini humo imeripoti.

Matangazo ya kibiashara

Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona imezidi milioni 2.3 nchini Brazil, na vifo 85,238 kwa ujumla vimerekodiwa, kulingana na takwimu za serikali.

Kutokana na mgogoro huo wa kiafya, jiji la Sao Paulo limeamua kuahirisha maadhimisho ya Carnival ambayo yangelifanyika mwezi Februari mwakani.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Meya wa Sao Paulo, Bruno Covas, amefahamisha kuwa maadhimisho hayo ya kijadi yananayohusisha mji wa Rio de Janeiro yatafanyika mwezi Mei au Julai mwakani.