MAREKANI-BRAZILI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Brazil na Marekani zarekodi vifo zaidi

Marekani na Brazil, nchi mbili zilizoathiriwa zaidi na janga la Corona zimethibitisha vifo vingi vinavyohusiana na ugonjwa hatari wa Covid-19 Jumatano wiki hii.

Raia wa Marekani wakiitikia zoezi la kufanyisha vipimo vya Covid-19, Julai 24, 2020 huko Miami Beach, Florida.
Raia wa Marekani wakiitikia zoezi la kufanyisha vipimo vya Covid-19, Julai 24, 2020 huko Miami Beach, Florida. AFP
Matangazo ya kibiashara

Marekani imerekodi vifo zaidi ya 150,000, na Brazil kwa upande wake imethibitisha vifo 90,000 vinavyohusiana na ugonjwa wa Covid-19.

Mlipuko huo ni mbaya sana katika nchi hii kubwa ya Amerika ya Kusini, ambayo inarekodi kwa wastani vifo zaidi ya 1,000 kwa siku kwa muda wa zaidi ya siku saba tangu mapema mwezi Julai.

Kwa upande wake, Marekani, ambayo ilitangaza mwishoni mwa mwezi wa Februari kifo chake cha kwanza kinachohusiana na Covid-19, imerekodi vifo 150,000 miezi mitano baadaye, idadi iliyo sawa na wakazi wa mji wa Savannah, huko Georgia.

Baada ya kupata nafuu mwishoni mwa kipindi cha baridi, Marekani inaona kuwa ugonjwa ho umeongezeka tena kwa kasi tangu mwishoni mwa mwezi Juni, hasa Kusini na magharibi mwa nchi, ambapo majimbo mengi yalilegeza masharti ya kudhibiti kusambaa kwa virusi vya Corona.