BRAZILI-CORONA-AFYA-UTALII

Coronavirus: Mipaka ya anga yafunguliwa tena kwa wageni Brazil

Brazil imechukuwa uamuzi wa kufungua tena mipaka yake kwa raia wa kigeni wanasafiri kwa ndege, kulingana na sheria ya rais iliyochapishwa kwenye Gazeti la serikali.

Brazil ilikuwa imefunga mipaka yake ya anga kwa wasafiri wa kigeni Machi 30 wakati ambapo janga la Corona lilikuwa likiathiri bara la Ulaya na Asia na lilikuwa limewasili huko Amerika Kusini.
Brazil ilikuwa imefunga mipaka yake ya anga kwa wasafiri wa kigeni Machi 30 wakati ambapo janga la Corona lilikuwa likiathiri bara la Ulaya na Asia na lilikuwa limewasili huko Amerika Kusini. EVARISTO SA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua ambayo inakusudia kufufua tasnia ya utalii ya Brazil iliyoathiriwa na janga la Corona. Brazil ambayo ni nchi ya pili ambayo imerekodi vifo vingi duniani kutokana na ugonjwa wa Covid-19, imethibitisha vifo zaidi ya 90,000 baada ya kurekodi vifo vipya 1,595 katika muda wa saa 24 zilizopita, Wizara ya Afya imetangaza.

Sheria hiyo imeongeza marufuku ya kuingia nchini humo kwa wageni wanasafiri kupitia nchi kavu au njia ya majini kwa kipindi cha siku 30. Lakini imebaini kwamba wageni wanaosafiri kwa kutumia njia ya anga "hawatopigwa marufuku tena". Wageni kutoka nchi za kigeni ambao watakaa siku 90 au chini ya siku hizo nchini Brazil watalazimika kutafuta cheti cha bima ya afya kwa kipindi chote watakuepo hapo.

Brazil ilikuwa imefunga mipaka yake ya anga kwa wasafiri wa kigeni Machi 30 wakati ambapo janga la Corona lilikuwa likiathiri bara la Ulaya na Asia na lilikuwa limewasili huko Amerika Kusini.

Tangu wakati huo imekuwa nchi ya pili iliyoathirika zaidi na virusi vya Corona baada ya Marekani na tasnia yake ya utalii imepata hasara kubwa ya dola milioni 23,6, kulingana na makadirio ya Shirikisho la Kitaifa la biashara, huduma na utalii (CNC).