MEXICO-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya vifo yapindukia 46,688, Mexico

Katika siku za hivi karibuni serikali ya Mexico ilisema kuwa idadi halisi ya watu walioambukizwa ni kubwa zaidi kuliko idadi ya kesi zilizothibitishwa.
Katika siku za hivi karibuni serikali ya Mexico ilisema kuwa idadi halisi ya watu walioambukizwa ni kubwa zaidi kuliko idadi ya kesi zilizothibitishwa. REUTERS

Mexico imerekodi vifo vipya 688 kutokana na mlipuko wa Corona katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, wizara ya afya imesema, na kufanya jumla ya vifo kufikia 46,688, ikiwa ni vifo vingi zaidi duniani baada ya Marekani na Brazil.

Matangazo ya kibiashara

Mexico kwa sasa inaongoza mbele ya Uingereza.

Rekodi ya kila siku ya 8,458 ya kesi mpya za maambukizi imethibitishwa pia na mamlaka nchini Mexico, kwa jumla ya visa 424,637 vya maambukizi vilivyothibitishwa.

Katika siku za hivi karibuni serikali ya Mexico iliesema kuwa idadi halisi ya watu walioambukizwa ni kubwa zaidi kuliko idadi ya kesi zilizothibitishwa.