MAREKANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Marekani yarekodi vifo zaidi ya 25,000 katika mwezi wa Julai

Katika Jimbo la Florida kulishuhudiwa kuongezeka kwa vifo vipya, na visa vipya zaidi ya 310,000 vya maambukizi, huko California na Texas (karibu kesi mpya 260,000).
Katika Jimbo la Florida kulishuhudiwa kuongezeka kwa vifo vipya, na visa vipya zaidi ya 310,000 vya maambukizi, huko California na Texas (karibu kesi mpya 260,000). REUTERS/Octavio Jones

Idadi ya vifo kutokana na janga la Corona nchini Marekani iliongezeka na kufikia zaidi ya 25,000 katika mwezi pekee wa Julai na idadi ya kesi zilizothibitishwa ilipanda mara dufu katika majimbo 19 nchini kote katika mwezi, kulingana na takwimu za shirika la habari la Reuters.

Matangazo ya kibiashara

Visa vipya Milioni 1,87 vya maambukizi vilithibitishwa katika mwezi wa Julai kote nchini, na kufikisha jumla ya idadi ya visa Milioni 4.5 vya maambukizi tangu kuzuka kwa janga hilo., ikiwa ni sawa na kuongezeka kwa 69%.

Idadi ya vifo iliongezeka kwa 20% katika mwezi Julai, sawa na karibu vifo 154,000 kwa jumla.

Katika Jimbo la Florida kulishuhudiwa kuongezeka kwa vifo vipya, na visa vipya zaidi ya 310,000 vya maambukizi, huko California na Texas (karibu kesi mpya 260,000).