MAREKANI-ANGA ZA JUU

Marekani: Chombo cha Dragon chatua duniani salama

Chombo cha Dragon kilichokuwa kimewabeba wanaanga hao wa kundi la Space X kilifika duniani katika ghuba ya Mexico Kusini mwa Pensacola, ghuba ya pwani ya Florida.
Chombo cha Dragon kilichokuwa kimewabeba wanaanga hao wa kundi la Space X kilifika duniani katika ghuba ya Mexico Kusini mwa Pensacola, ghuba ya pwani ya Florida. JOE RAEDLE / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / GETTY IMAGES VIA AFP

Kikosi cha wanaanga kutoka Marekani kuwahi kuzuru  anga za mbali  katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, kimerejea na kutua nyumbani salama.

Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huo ulifanywa na wanaanga wa kikundi cha Space X kikishirikiana na kitengo cha utafiti wa maswala ya anga na sayansi nchini humo na kudhihirisha uwezo wa nchi hiyo kuhudumu na kuwatuma wanasayansi wao kwenda  dunia ya anga za mbali na kurudi.

Uwezo huu ulipotea wakati nchi hiyo ilipoacha kutumia vyombo vyake vya safari za anga za mbali mwaka 2011.

Chombo cha Dragon kilichokuwa kimewabeba wanaanga hao wa kundi la Space X kilifika duniani katika ghuba ya Mexico Kusini mwa Pensacola, ghuba ya pwani ya Florida.

Hii ni mara kwanza timu iliyokwenda anga za mbali kuwasili katika bahari ya Marekani tangu wakati wa chombo cha Apollo miaka 45 iliyopita.

Wakati huo huo rais wa Marekani Donald Trump amepongeza kurejea kwa ujumbe huo salama.

Kampuni kubwa ya utengenezaji wa vifaa vya anga za mbali ya Boeing ina mkataba na NASA kujaribu kuwabeba wanaanga katika kituo cha anga za mbali kwa ndege yake ya anga- CST-100 Starliner spacecraft. Pia imeweza kutengeneza kitengo cha hewa kwa ajili ya kuwalinda wanaanga katika nyakati muhimu za kuondoka na kuingia tena ndani ya chombo.