MAREKANI-CORONA-AFYA-SIASA

Marekani: Mazungumzo juu ya mpango wa msaada kukabiliana na Corona yaanza

Wabunge kutoka vyama vya Democratic na Republican bado wamegawanyika kwa mpango huo mpya wa msaada wa kukabiliana na Corona.
Wabunge kutoka vyama vya Democratic na Republican bado wamegawanyika kwa mpango huo mpya wa msaada wa kukabiliana na Corona. REUTERS

Shinikizo linaendelea kuongezeka nchini Marekani kwa wabunge kutoka vyama vya Democratic na Republican ili kufikia makubaliano juu ya mpango wa kusaidia uchumi dhidi ya janga la Corona wakati mpango wa kipekee wa fidia kwa wasio na ajira umefika ukingoni.

Matangazo ya kibiashara

Wabunge kutoka chama cha democratic, ambao ni wengi katika Baraza la Wawakilishi, na wawakilishi wa wengi wa chama cha Republican katika Bunge la Seneti wanatarajia leo Jumatatu kuanza tena mazungumzo katika makao makuu ya Bunge kwa minajili ya kuongeza muda wa hatua za kufaidi mamilioni ya Wamarekani wasio na kazi.

Kambi hizo mbili bado zimegawanyika kwa mpango huo mpya wa msaada.

Mazungumzo yatajikita hasa kwa posho maalum ya serikali ya dola 600 kwa wiki ambayo iliwekwa na ambayo muda wake ulimalizika siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita.

Wabunge kutoka chama cha Democratic wanakataa kusalimu amri kwenye suala hilo na wanataka Baraza la Congress kuongeza muda wa hatua hiyo ambayo, kwa macho yao, imekuwa njia ya kuishi kwa mamilioni ya Wamarekani walioathirika na ukosefu wa ajira wakati wa mgogoro wa kiafya.

Wanasisitiza kwamba mpango wa msaada kwa umma uwe wa karibu dola bilioni 1,000.

White House na wabunge wa chama cha Republican, kwa upande wao, wanasema mpango huo ni wa gharama kubwa na wanataka posho za shirikisho za kila wiki zipunguzwe, wakisema hawawahimiza watu wasio na kazi kutafuta kazi kwa bidii.