MAREKANI-CORONA-AFYA-SIASA

Wataalam waonya Marekani kuchukuwa hatua zaidi dhidi ya Corona

Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence wakati anaongoza mkutano wa kikosi kazi kuhusu ugonjwa wa Covid-19 huko Washington Julai 8, 2020.
Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence wakati anaongoza mkutano wa kikosi kazi kuhusu ugonjwa wa Covid-19 huko Washington Julai 8, 2020. REUTERS/Carlos Barria

Watalaam wa afya katika Ikulu ya Marekani wanaonya kuwa maambukizi ya virusi vya corona, yanaendelea kuongezeka kwa kasi nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Maambukizi nchini Marekani, yamefikia zaidi ya Milioni 4.6 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 150,000.

Daktari Deborah Birx, mtalaam wa afya katika Ikulu ya White House ametoa wito kwa raia wa Marekani kuendelea kuchukua tahadhari na kuvaa barakoa.

Hayo yanajiri wakati visa Milioni 18 vya maambukizi vimeripotiwa kote duniani, baada ya visa Laki 2 na Elfu 64 kuthiobitishwa na wagonjwa Milioni 10.7 wamepona ugonjwa wa Covid-19.

Idadi ya vifo imefikia Laki 6 na Elfu 89, baada ya vifo vipya 5,901 kuthibitishwa.

Mwishoni mwa wiki hii iliyopita Shirika la Afya duniani WHO lilionya kuwa janga la virusi vya Corona litadumu kwa muda mrefu na huenda likasababisha ''kuelemewa kwa mikakati ya kukabiliana nalo”.