MAREKANI-MAJANGA YA ASILI

Kimbunga Isaias : Jimbo la Carolina Kaskazini lawekwa katika hali ya dharura

Barabara iliyojaa maji kutokana na mafuriko baada ya kimbunga Florence kupiga huko Clinton, Carolina Kaskazini, Septemba 15, 2018.
Barabara iliyojaa maji kutokana na mafuriko baada ya kimbunga Florence kupiga huko Clinton, Carolina Kaskazini, Septemba 15, 2018. REUTERS/Eduardo Munoz

Wakazi wa majimbo ya Carolina Kusini na Kaskazini nchini Marekani wameonywa kuanza kuchukua tahadhari kutokana na kimbuga Isaias, kinachoelekea eneo la Pwani ya Mashariki mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Watalaam wanaoshughulikia masuala ya kimbunga wanaonya kuwa, kimbunga hicho kinatarajiwa kufika katika maeneo hayo kuanzia leo.

Hata hivyo, watalaam hao wanasema huenda kimbunga hicho kisiwe na nguvu kubwa baada ya kuanzia katika visiwa vya Carribean na kusabababisha vifo vya watu wawili.

Kimbunga Isaias ni cha tisa tangu kuanza kwa mwaka huu, na sasa Mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa inaonya pia kuwa, kimbunga hiki kitasabbisha mvua kubwa eneo la Mashariki katika Pwani ya Marekani.

Tayari Gavana wa Jimbo la Carolina Kaskazini Roy Cooper ametangaza hali ya dharura kwa hofu ya kutokea kwa kimbunga hicho.