MAREKANI-MAZUNGUMZO-CORONA-UCHUMI

Marekani: Mazungumzo yaendelea kuhusu mpango wa msaada kukabiliana na Corona

Capitol ni jengo ambalo hutumika kama makao makuu ya Bunge la Congress huko Washington, D.C.
Capitol ni jengo ambalo hutumika kama makao makuu ya Bunge la Congress huko Washington, D.C. REUTERS/Kevin Lamarque

Wabunge kutoka vyama vya Democratic na Republican nchini Marekani wanatarajia kuendelea na mazungumzo yao leo Jumanne huko Washington kuhusu kuongeza muda wa mpango wa faida ya ukosefu wa ajira kama sehemu ya mpango wa kunusuru uchumi wa Marekani dhidi ya janga hilo.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya siku kadhaa za mazungumzo, kambi hizo mbili bado zimegawanyika wakati muda wa hatua za kuwanufaisha mamilioni ya Wamarekani wasio na ajira ulifikia kikomo Ijumaa ya wiki iliyopita.

"Tumepiga hatua kubwa kuhusu maswala kadhaa, " Kiongozi wa wachache katika Bunge la Seneti, Chuck Schumer, amewaambia waandishi wa habari baada ya mazungumzo ya Jumatatu wiki hii. "Kuna maswala mengi ambayo hayajapatiwa ufumbuzi", ameongeza.

Mwenyekiti wa Hifadhi ya Shirikisho la Chicago Charles Evans Jumatatu aliwataka wabunge na Ikulu ya White House kukubaliana juu ya kuongeza matumizi ya serikali ili kusaidia uchumi wa Marekani ambao athari za mgogoro wa kiafya zimesababisha mamia ya mamilioni ya watu kukosa ajira.

Mazungumzo kati ya wabunge kutoka vyama vya Democratic na Republican yamekwamia hasa kwenye ugawaji maalum wa posho ya Dola 600 kwa wiki ambayo wabunge kutoka cha Democratic wanataka ifanyiwe marekebisho, huku maseneta kutoka chama cha Republican wakiona kuwa kiwango hicho ni kikubwa na kitazorotesha uchumi wa nchi.