MAREKANI-BIDEN-HARRIS-MAREKANI

Harris aambatana na Biden kwa mara ya kwanza katika kampeni za uchaguzi

Seneta Kamala Harris kwa mara ya kwanza ameshirikiana na Joe Biden katika kampeni ya uchaguzi, Agosti 12 huko Wilmington.
Seneta Kamala Harris kwa mara ya kwanza ameshirikiana na Joe Biden katika kampeni ya uchaguzi, Agosti 12 huko Wilmington. REUTERS/Carlos Barria

Mgombea urais kupitia chama che Democratic nchini Marekani Joe Biden na mgombea mwenza wake Kamala Harris kwa pamoja wamezindua kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Novemba.

Matangazo ya kibiashara

Hii imekuja siku moja baada ya Biden kumteua Bi. Harris kuwa mgombea mwenza, na wawili hao wamemwelezea raia Donald Trump kama kiongozi asiyejua uongozi na aliyeiharibu Marekani.

Harris alianza kumshambulia Trump akisema amewaingiza hatarini Wamarekani kwa kushindwa kulichukulia kwa umakini janga la Corona na kuitumbukiza Marekani kwenye mzozo wa kiuchumi, katika wakati ambapo inapambana na kukosekana kwa usawa wa rangi na kijamii.

Nae Joe Biden amesema serikali yake na Kamala Harris itakuwa na mkakati thabiti wa kukabiliana na Covid-19 utakaobadilisha hali ya mambo.

“Uvaaji wa barakoa, kuongeza upimaji na kuziwezesha serikali za majimbo ili kufungua shule na biashara kwa usalama. Tunaweza. Tunachohitaji ni rais na makamu walio tayari kuongoza na kuwajibika", alisema Biden.

Hata hivyo, rais Trump amemuelezea Bi. Harris kama mtu aliyeanguka kama jiwe baada ya kushindwa katika uteuzi wa kuwa mgombea urais wa chama chake cha Democratic.