MAREKANI-BIDEN-SIASA

Marekani: Chama cha Democratic kumuidhinisha rasmi Biden kuwa mgombea urais

Joe Biden, amemteua Kamala Harris kuwa mgommbea mwenza kupeperusha bendera ya chama cha Democratic.
Joe Biden, amemteua Kamala Harris kuwa mgommbea mwenza kupeperusha bendera ya chama cha Democratic. REUTERS/Mike Blake

Mkutano Mkuu wa siku nne wa chama cha Democratic nchini Marekani umeanza Jumanne wiki hii kwa njia ya mtandao kwa lengo la kumwidhinisha rasmi Joe Biden kuwa mgombea urais kupambana na rais anaye maliza muda wake Donald Trump mwezi Novemba.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu unafanyika kwa njia ya mtandao kwa sababu ya janga la Corona.

Ratiba inaonesha kuwa uteuzi rasmi wa Biden utafanyika siku ya Alhamisi, ambapo kwenye hotuba yake anatazamiwa kuzungumzia dira yake ya kuiunganisha Marekani na kuitowa kwenye machafuko na mzozo wa sasa, kwa mujibu wa chama chake

Mwanasiasa mkongwe Bernie Sanders ambaye amewahi kutia nia ya kutaka kugombea kupitia chama hiki, amekuwa miongoni mwa wazungumzaji wa kwanza katika mkutano huu.

Katika orodha ya wazungumzaji wamo pia marais wa zamani Barack Obama na Bill Clinton na wanamuziki Billie Eilish na John Legend watakaotumbuiza.

Siku ay Jumatatu Sanders alisema kwamba ni jambo la lazima kwa Wamarekani kumshinda Donald Trump kwenye uchaguzi wa mwaka huu.

Miongoni mwa wazunguzaji wengine katika mkutano huu ni Michel Obama, mke wa rais wa zamani Barack Obama.

Hotuba za Joe Biden, mgombea mwenza wake Kamala Harris, na vigogo wengine wa chama cha Democratic zitarushwa kuanzia saa 7:00 hadi saa 9:00 mchana kila siku kuanzia leo hadi Agosti 20.