MAREKANI-MAJANGA YA ASILI

Marekani: Watu 175,000 wahamishwa kufuatia mkasa wa Moto California

Californie yakumbwa na mkasa wa moto wa nyika.
Californie yakumbwa na mkasa wa moto wa nyika. Justin Sullivan/Getty Images/AFP

Moto wa nyika uliosababishwa na radi huko California umesababisha uharibu mkubwa, ambapo watu 175,000 wamelazimika kuhamishwa na kupelekwa maeneo salama.

Matangazo ya kibiashara

Idadi ya vifo imeongezeka hadi sita na watu 43 wamejeruhiwa, na majengo mengi yameharibiwa. Moto huo, uliosambaa kwa zaidi ya nyumba 370, umechukua ukubwa wa eneo mara mbili kwa ule wa Los mji wa Angeles.

Migurumo ya radi ambayo ilisababisha moto huo katika mashamba na misitu iliyokauka kutokana na joto kali imesababisha uharibifu usiyokuwa wa kawaida kwa karibu miongo miwili, huku ikikadiriwa visa 11,000 vya uharibifu uliosababishwa na radi.

"Ikiwa huna uhakika kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, njoo California," Gavana Gavin Newsom alisema siku ya Alhamisi jioni katika Mkutano Mkuu wa chama cha Democratic.

Matukio kadhaa yaliyosababishwa na Moto huo yamripotiwa katika eneo la San Francisco Bay Area, hasa Mashariki mwa mji wa Palo Alto na katika eneo moja Kusini mwa Sacramento.