MEXICO-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya vifo yapindukia zaidi ya 60,000 Mexico

Pamoja na vifo 60,800, Mexico ni nchi ya tatu kwa suala la vifo vinavyohusiana na Corona.
Pamoja na vifo 60,800, Mexico ni nchi ya tatu kwa suala la vifo vinavyohusiana na Corona. REUTERS/Carlos Jasso

Mexico imerekodi visa vipya 3,451 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo vipya 320 katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, wizara ya afya ya Mexico imetangaza.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na ripoti kuhusu janga hilo nchini Mexico, idadi ya visa vya maambukizi imefikia 563,705 na vifo 60,800. Katika siku za hivi karibuni serikali ya Mexico ilisema kuwa idadi halisi ya watu walioambukizwa ni kubwa zaidi kuliko idadi ya kesi zilizothibitishwa.

Hivi karibuni Shirika la Afya Duniani, WHO, limeaonya kuwa licha ya jitihada zinazofanyika kutafuta chanjo na dawa ya kupambana na janga la virusi vya Corona, huenda kusiwe na suluhu ya muda mrefu ya kukabiliana na janga hili.

WHO imezitaka nchi zote kutilia mkazo hatua za kuzuia kusambaa kwa virusi.

Hata hivyo WHO imeendelea kukosoa hatua zilizochukuliwa hivi karibuni na baadhi ya nchi duniani kwa kulegeza masharti ya kukabiliana na janga la Covid-19, ikisema kuwa Covid-19 bado ni tishio duniani.