MAREKANI-SIASA-USALAMA

Marekani 2020: Pence aonya juu ya hatari za usalama ikiwa Biden atashinda uchaguzi

Mike Pence atolea wito Wamarekani kumpigia kura Donald Trump katika uchaguzi wa urais wa Novemba 3, akionya kuwa ushindi wa Joe Biden ni hatari kwa usalama wa Marekani.
Mike Pence atolea wito Wamarekani kumpigia kura Donald Trump katika uchaguzi wa urais wa Novemba 3, akionya kuwa ushindi wa Joe Biden ni hatari kwa usalama wa Marekani. REUTERS

Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence amebaini katika Mkutano Mkuu wa chama cha Republican Jumatano wiki hii kwamba kuchaguliwa kwa Donald Trump ni muhimu kwa usalama wa nchi na ukuaji wa uchumi.

Matangazo ya kibiashara

Bw. Pence amesema kuwa ushindi wa Joe Biden unaweza kuitumbukiza Marekani katika machafuko ya hali ya juu na kusababisha mdororo wa uchumi.

Wakati Marekani ikiendelea kukumbwa na maadamano kufuatia kisa cha polisi kumpiga risasi mtu mweusi huko Wisconsin, wajumbe katika Mkutano huo Mkuu wa chama cha Republican wameelezea uchaguzi wa Novemba 3 kati ya Donald Trump na Joe Biden kama chaguo kati ya amani au usalama na machafuko.

"Ukweli tu ni kwamba, hamtakuwa na usalama nchini Marekani ikiwa Joe Biden atashinda uchaguzi," Mike Pence amesema mbele ya umati uliokusanyika Fort McHenry huko Baltimore, Maryland.