MAREKANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Visa milioni 6 vya maambukizi zathibitishwa Marekani

Karibu watu 183,000 wamefariki kutokana na janga hatari la Covid-19 Marekani.
Karibu watu 183,000 wamefariki kutokana na janga hatari la Covid-19 Marekani. REUTERS/Jeenah Moon

Idadi ya visa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Marekani imeongezeka hadi Milioni sita, kulingana na takwimu za shirika la habari la REUTERS, wakati majimbo mengi ya Midwest yanakabiliwa na ongezeko la maambukizi.

Matangazo ya kibiashara

Marekani ni nchi yenye idadi kubwa ya watu walioambukizwa virusi vya Corona Duniani. Pia imerekodi idadi kubwa ya vifo. Karibu watu 183,000 wamefariki kutokana na janga hatari la Covid-19.

Wakati New York, California na majimbo ya kusini kama Texas ni kitovu cha milipuko hiyo mikuu hapo awali, huku Iowa, Dakota ya Kaskazini na Dakota ya Kusini na Minnesota ni majimbo ambayo yamerekodi idadi kubwa ya kila siku ya maambukizi ya Corona. Montana na Idaho hawajawahi kuwa na wagonjwa wengi katika hospitali kutokana na Covid-19, ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona

Kati ya kesi mpya zilizogunduliwa huko Iowa, nyingi ziko katika kaunti zilizo na maeneo ya Chuo Kikuu cha Iowa au Chuo Kikuu cha Jimbo la Iowa.

Katika nchi nzima, shule za upili na vyuo vikuu vimejikuta idadi ya maambukizi ikiongezeka kutokana na kurejea kwa wanafunzi katika mabweni, hali ambayo ilisababisha baadhi ya wanafunzi kufuata visomo kupitia intaneti.