MEXICO-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya maambukizi yakaribia 600,000 Mexico

Serikali ya Mexico ilionya hapo awali kuwa idadi halisi ya watu walioambukizwa huenda ikawa kubwa.
Serikali ya Mexico ilionya hapo awali kuwa idadi halisi ya watu walioambukizwa huenda ikawa kubwa. REUTERS/Carlos Jasso

Mexico imerekodi visa vipya 3,719 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo vipya 256 katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, wizara ya afya imesema.

Matangazo ya kibiashara

Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona nchini Mexico sasa imefikia 599,560 na vifo 64,414. Serikali ilionya hapo awali kuwa idadi halisi ya watu walioambukizwa huenda ikawa kubwa.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwezi Desemba 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.