MAREKANI-MAUAJI-HAKI

Marekani: Trump atetea mtuhumiwa wa mauaji ya Kenosha

Rais wa Marekani Donald Trump wakati wa hotuba yake ya kuapishwa kama mgombea wa urais Agosti 27, 2020 Ikulu ya White House.
Rais wa Marekani Donald Trump wakati wa hotuba yake ya kuapishwa kama mgombea wa urais Agosti 27, 2020 Ikulu ya White House. CHIP SOMODEVILLA / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / Getty Images via

Rais wa Marekani Donald Trump ameamua kumtetea mtuhumiwa wa miaka 17 anayedaiwa kuua watu wawili wakati wa maandamano huko Kenosha, katika jimbo la Wisconsin, wiki iliyopita, akisema mshukiwa alikuwa akijaribu kukimbia na angeliuawa na waandamanaji kama hangelifanya hivyo.

Matangazo ya kibiashara

Donald Trump amepanga leo Jumanne kuzuru mji huo wenye wakaazi 100,000 unaopatikana Kusini mwa Milwaukee karibu na Ziwa Michigan ambapo maandamano yalizuka baada ya afisa wa polisi kumjeruhi vibaya mtu mweusi, Jacob Blake, Agosti 23, kwa kumpiga risasi saba mgogoni.

Wakati wa usiku wa tatu wa maandamano, Kyle Rittenhouse aliwafyatulia risasi waandamanaji watatu akitumia bunduki ya kivita, na kuua wawili kati yao.

"Alikuwa akijaribu kuwatoroka [...] Na kisha akaanguka na wakaanza kumshambulia," Donald Trump amesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye Ikulu ya White House. "Nadhani alikuwa katika hatari kubwa (...) Labda angeuawa," ameongeze rais wa Marekani akijaribu kumtetea kijana huyo mwenye umri wa miaka 17.

Kyle Rittenhouse ameshtakiwa kwa makosa mawili ya mauaji ya na kujaribu kuua. Wakili wake ambaini kwamba anatarajia kuonyesha kuwa mteja wake alikuwa amejihami baada ya kuvamia na kundi la waandamanaji.

Donald Trump, aliyeteuliwa rasmi wiki iliyopita kama mgombea wa Chama cha Republican kwa uchaguzi wa urais wa Novemba amekataa kulaani vitendo vya vurugu vilivyofanywa na wafuasi wake na amepinga dhidi ya kile alichokielezea kama ghasia na uasi unaofanywa na waandamanaji "kutoka mrengo wa kushoto".

Makamu wa Rais wa zamani, Joe Biden, mpinzani wa Donald Trump kutoka chama cha Democratic, katika uchaguzi wa Novemba 3, almemshtumu rais anayemaliza muda wake kwa kuchochea vurugu akitumia maneno yake, huku akibaini kwamba wahalifu na waporaji wanapaswa kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Ikulu ya White House imebaini kwamba Donald Trump hajapanga kukutana na familia ya Jacob Blake wakati wa ziara yake huko Kenosha. Rais atatathmini uharibifu uliofanywa na waandamanaji na atakutana na wafanyabiashara, White House imsema.