BRAZILI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya visa vya maambukizi yapindukia zaidi milioni 4 nchini Brazil

Idadi ya vifo vya kila siku imeanza kupungua kidogo, wakati zaidi ya watu 124,000 tayari wamepoteza maisha nchini Brazil.
Idadi ya vifo vya kila siku imeanza kupungua kidogo, wakati zaidi ya watu 124,000 tayari wamepoteza maisha nchini Brazil. REUTERS/Ueslei Marcelino

Brazil, nchi ya pili duniani yenye vifo vingi vinavyohusiana na ugonjwa hatari wa COVID-19, imerekodi visa zaidi ya Milioni nne vya maambukizi ya ugonjwa huo, wakati kamati ya wataalam huru imeanza uchunguzi juu ya usimamizi wa janga hilo.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Alhamisi, Brazili ilikuwa na visa 4,041,638 vya maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa COVID-19. Lakini idadi ya vifo vya kila siku imeanza kupungua kidogo, wakati zaidi ya watu 124,000 tayari wamepoteza maisha.

"Huu ni mwanzo wa kile tunatarajia kuwa ni kuanza kushuka kwa idadi ya vifo, lakini bado ni mwanzo, tuyendelee kusubiri, tusikate tu tamaa," Mauro Sanchez, mtaalam wa magonjwa katika Chuo Kikuu cha Brasilia, ameliambia shirika la habari la AFP.

Janga hilo limeuwa watu wasiopungua 864,510 duniani kote tangu mwishoni mwa mwezi Desemba ulipoanzia huko Wuhan nchini China, kulingana na ripoti iliyotolewa na shirika la habari la AFP kutoka vyanzo rasmi.

Marekani ni nchi iliyoathirika zaidi kwa vifo na visa vya maambukizi, ambapo vifo 187,000 vimeripotiwa kwa jumla ya visa Milioni 6.1, kulingana na takwimu za Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.