MAREKANI-CORONA-AFYA-SIASA

Coronavirus: Trump amlaumu mpinzani wake kuhusu kauli yake dhidi ya chanjo

Trump amesema mpinzani wake anatia siasa katika suala hilo.
Trump amesema mpinzani wake anatia siasa katika suala hilo. AP/Evan Vucci

Rais wa Marekani Donald Trump kwa mara nyingine, amebashiri kuwa chanjo ya kupambana na virusi vya Corona itapatikana kabla ya Uchaguzi Mkuu mwezi Novemba.

Matangazo ya kibiashara

Kauli ya rais Trump imekuja baada ya mpinzani wake katika Uchaguzi huo Joe Biden kusema kuwa uongozi wa Trump hautegemewi kutoa chanjo inayoaminiwa na Wamarekani.

Hata hivyo, Trump amesema mpinzani wake anatia siasa katika suala hilo.

Marekani ina maambuikzii zaidi ya Milioni Sita.

Mapema wiki iliyopita vituo vya vya kudhibiti na kuzuia maambukizi ya magojnwa nchini Marekani (CDC) viliwataka maafisa wa afya wa majimbo yote nchini humo kuwa tayari kusambaza chanjo dhidi ya Corona kwa watu walio katika hatari kubwa mwishoni mwa mwezi Oktoba.

Hivi karibuni Anthony Fauci, mtaalam anayeongoza wa magonjwa ya kuambukiza nchini Marekani, aliiambia televisheni ya MSNBC kwamba, kulingana na takwimu kutoka kwa vipimo vinavyoendelea, takwimu za kliniki za kutosha zinaweza kupatikana mwezi Novemba au Desemba ili kubaini kama moja ya chanjo iko salama na nzuri.

Kulingana na nyaraka zilizochapishwa na Gazeti la New York Times, CDC inajiandaa kuwa na chanjo moja au mbili kwa idadi ndogo mwishoni mwa mwezi Oktoba.