MAREKANI-CHINA-USHIRIKIANO

Marekani yafuta zaidi visa 1,000 za raia wa China

Uhusiano kati ya Marekani na China umeendelea kuzorota.
Uhusiano kati ya Marekani na China umeendelea kuzorota. Greg Baker / AFP

Marekani, kuanzia wiki hii, imefuta zaidi ya visa 1,000 za raia kutoka China, msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo amesema.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo ni sehemu ya jaribio la utawala wa Trump kuzuia kuingia nchini Marekani wanafunzi na watafiti kutoka China wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na jeshi la China.

Katika tangazo lake la mwezi Mei, rais wa Marekani Donald Trump alipiga marufuku watafiti na wanafunzi kutoka China kuingia nchini marekani, akisema Beijing ilikuwa ikiwatumia kupata teknolojia nyeti ya Marekani na elimu ya nchi hiyo.

Wizara ya Mambo ya Nje ilianza kutekeleza sheria hizi Juni 1.Idara hiyo ina mamlaka ya kubatilisha visa, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ameongeza, huku akibaini kwamba wizara hiyo itatekeleza sheria hizo wakati itapokea taarifa zinazobaini kwamba mwenye visa anaweza kupigwa marufuku kuingia nchini marekani au kwamba anaweza kupata au la visa.Hakutoa maelezo ya nani amebatilishwa visa.

Hakutoa maelezo kuhusu watu ambao visa zao vimebatilishwa.