VENEZUELA-MAREKANI-USALAMA

Venezuela: Maduro atangaza kukamatwa kwa 'jasusi wa Marekani'

Rais wa venezuela, Nicolas Maduro.
Rais wa venezuela, Nicolas Maduro. REUTERS/Manaure Quintero

'Jasusi wa Marekani' amekamatwa karibu na viwanda vya kusafishia mafuta nchini Venezuela baada ya mamlaka kutibua mpango uliolenga kusababisha "mlipuko" katika kiwanda kingine cha mafuta, rais wa Venezuela Nicolas Maduro amesema.

Matangazo ya kibiashara

"Tulimkamata jana (...) afisa wa upelelezi wa Marekani ambaye alikuwa akifanya kazi yake ya upelelezi, katika Jimbo la Falcon, 'kwenye viwanda vya mafuta vya Amuay na Cardon', huo Paragwaana (kaskazini magharibi), amesema rais Maduro katika hotuba iliyorushwa kwenye runinga ya serikali.

Sio mara ya kwanza Caracas kutangaza kuwakama maafisa wa Marekani nchini venezuela.

Mapema mwezi Mei, rais wa Venezuela alitangaza kwamba mamlaka ya nchi yake iliwakamata "magaidi" 13, ikiwa ni pamoja na raia wawili wa Marekani ambao aliwataja kuwa ni mamluki, kwa kuhusika kwao katika jaribio lililotibuliwa, ambalo alisema lengo lake ilikuwa kumuondoa madarakani.

Hivi karibuni Makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence, alitangaza hatua mpya za kuhamasisha jeshi la Venezuela kutoendelea kumuunga mkono rais wa Venezuela Nicolas Maduro.

Marekani imeendelea kumuunga mkono na kutangaza kwamba inamtambua kama rais wa Marekani Juan Guaido, mpinzani na mkosoaji mkubwa wa rais Nicolas Maduro.

Mwezi wa Julai Marekani ilichukuwa vikwazo dhidi ya mkuu wa Mahakama Kuu ya Venezuela Maikel Moreno na kutangaza fidia ya dola milioni 5 kwa taarifa yoyote itakayohusiana na kukamatwa kwake au kushtakiwa kwa madai ya kuhusika kwake katika uhalifu wa kimataifa.