MAREKANI-CORONA-AFYA

CDC: Zaidi ya watu 193,000 wamefariki kutokana na Corona Marekani

Marekani ni nchi iliyoathiriwa zaidi na janga la Covid-19 duniani.
Marekani ni nchi iliyoathiriwa zaidi na janga la Covid-19 duniani. REUTERS/Stefan Jeremiah

Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) nchini Marekani vimerekodi vifo vipya 807 kutokana na virusi vya Corona na kufikisha idadi ya vifo kufikia 193,195.

Matangazo ya kibiashara

Vituo hivyo pia vinasema vimerekodi visa vipya 40,423 vya maambukizi na kufanya idadi ya maambukizi nchini Marekani kufikia 6,467,481.

Takwimu hizi ziliripotiwa Septemba 12. Kesi zote zinazoripotiwa na mamlaka ya kila Jimbo hazitiliwi maaanani.

Hayo yanajiri wakati Shirika la Afya Duniani, WHO, linabaini kwamba idadi ya visa vipya imeongezeka duniani.

Idadi ya kila siku ya maambukizi ya virusi vya Corona duniani imefikia rekodi mpya kwa visa 307,930, Shirika la Afya duniani, WHO, limethibitisha.

Ongezeko kubwa zaidi limeonekana nchini India, Marekani na Brazil. India imerekodi visa vipya 94,372, Marekani visa vipya 45,523 na Brazil visa vipya 43,718, WHO imebaini kwenye wavuti yake.

Janga hilo pia limesababisha vifo vipya 5,537 katika muda wa saa 24 zilizopita, na kufanya idadi ya vifo duniani kufikia 917,417.