MAREKANI-TRUMP-BIDEN-SIASA

Biden: Trump alitakiwa kujiuzulu baada ya kushindwa kuonesha uongozi katika mapambano dhidi Corona

Trump ambaye ametofautiana na Biden kuhusu namna ya kukabiliana na janga hili, amekuwa akisema chanjo ya Corona huenda ikapatikana hivi karibuni.
Trump ambaye ametofautiana na Biden kuhusu namna ya kukabiliana na janga hili, amekuwa akisema chanjo ya Corona huenda ikapatikana hivi karibuni. AP Photo/Patrick Semansky

Mgombea urais kupitia chama cha Democratic nchini Marekani Joe Biden amesema rais Donald Trump alistahili kujiuzulu kutokana na kile alichosema ameshindwa kuonesha uongozi katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona ambapo watu zaidi ya Milioni Sita wameambukizwa na wengine karibu Laki Mbili wamefariki dunia.

Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Biden imekuja baada ya rais Trump, kutofautiana na Robert Redfield, kiongozi wa taasisi ya kuzuia magonjwa nchini humo CDC.Wiki hii rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kwamba angalau dawa milioni 100 ya chanjo dhidi ya Corona zinaweza kusambazwa nchini Marekani ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, akipingana na kauli ya mkurugenzi wa Vituo vya kuzuia na Kudhibiti magonjwa nchini humo (CDC).

Siku ya Jumatano, Robert Redfield alisema kuwa chanjo ijayo ya Corona inaweza kutolewa kwa idadi kubwa katikati ya mwaka wa 2021 au mapema kidogo.

"Alifanya makosa aliposema hivyo," alibaini Donald Trump, na kuongeza mbele ya waandishi wa habari kwamba alizungumza kwa simu na Robert Redfield. "Nadhani alikuwa amechanganyikiwa. Labda hakuelewa swali hilo," ameongeza rais wa Marekani, ambaye hivi karibuni aliidhinishwa na chama chake cha Republican kupeperusha bendera yake katika uchaguzi wa urais ambao umepangwa kufanyika Novzmba 3.

Trump ambaye ametofautiana na Biden kuhusu namna ya kukabiliana na janga hili, amekuwa akisema chanjo ya Corona huenda ikapatikana hivi karibuni.