MAREKANI-BIDEN-TRUMP-SIASA-HAKI

Uteuzi wa jaji mpya wa Mahakama ya Juu: Biden amtaka Trump kuheshimu Katiba ya Marekani

Biden anawataka Maseneta kukataa uteuzi wa rais Trump.
Biden anawataka Maseneta kukataa uteuzi wa rais Trump. REUTERS/Alan Freed

Mgombea wa urais kupitia chama cha Democratic nchini Marekani, amemkosoa rais Donad Trump kuahidi kufanya uteuzi wa Jaji mpya wa Mahakama ya Juu wiki ijayo, baada ya kifo cha Ruth Bader Ginsburg wiki iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Biden amesema kitendo cha rais Trump ni ukiukwaji wa Katiba ya Marekani, na uteuzi huo unatashili baada ya uchaguzi Mkuu wa mwezi Novemba.

Biden anawataka Maseneta kukataa uteuzi wa rais Trump.

Rais Donald Trump ameahidi kumteuwa mwanamke wiki ijayo kujaza nafasi iliyowachwa wazi kufuatia kifo cha Jaji Ruth Bader Ginsburg, na kuishinikiza Seneti linalodhibitiwa na Warepublican kuidhinisha haraka jina hilo.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni jimboni North Carolina, Rais Donald Trump alisema atamteuwa mrithi wa Ginsburg licha ya kupingwa na Wademocrat, akiongeza kuwa kwa sasa hajui ni nani atakayemteuwa.

Wajumbe wa Republican wanataka mrithi wa Jaji Ginsburg apatikane kabla ya uchaguzi, huku Wademocrat wakisisitiza kuwa uamuzi huo utafanywa na rais atakayechaguliwa Novemba 3.

Kwa mujibu wa duru ya shirika la habari la Reuters, orodha rais donald Trump ya majina yanayoweza kuteuliwa inawajumuisha majaji wawili wanawake, Amy Coney Barret na Barbara Lagoa.