MAREKANI-TRUMP-HAKI-SIASA

Donald Trump: Kufikia Jumamosi, nitakuwa nimemteua Jaji wa Mahakama ya Juu.

Rais wa Marekani Donald Trump.
Rais wa Marekani Donald Trump. REUTERS/Mike Segar

Rais wa Marekani Donald Trimp, amesema atamteua Jaji wa Mahakama ya Juu kufikia siku ya Jumamosi, kuchukua nafasi ya Ruth Bader Ginsburg aliyefariki dunia wiki iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Trump amedokeza kuwa anatarajia kumtea mwanamke na kuwataka Masesenta wa chama cha Republican kumwidhinisha.

Hata hivyo, mipango ya rais Trump, inapigwa vikali na mgombea wa urais kupitia chama cha Democratic Joe Biden, anayetaka uteuzi huo kufanyika baada ya Uchaguzi wa mwezi Novemba.

Biden amewataka Maseneta wa Republican kukataa uteuzi wa Trump, suala ambalo huenda lisifanikiwe kwa sababu chama cha Republican kina viti vingi katika Bunge la Seneti nchini Marekani dhidi ya chama cha Democratic.

Wajumbe wa Republican wanataka mrithi wa Jaji Ginsburg apatikane kabla ya uchaguzi, huku Wademocrat wakisisitiza kuwa uamuzi huo utafanywa na rais atakayechaguliwa Novemba 3.

Kwa mujibu wa duru ya shirika la habari la Reuters, orodha rais donald Trump ya majina yanayoweza kuteuliwa inawajumuisha majaji wawili wanawake, Amy Coney Barret na Barbara Lagoa.