Coronavirus: Idadi ya vifo yapindukia laki mbili Marekani
Imechapishwa:
Idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Marekani kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona, sasa imeongezeka na kufikia zaidi ya Laki Mbili, kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.
Pamoja na vifo hivyo, watu wengine Milioni Sita na Laki Nane, wameambukizwa virusi hivyo na kuifanya Marekani kuwa nchi yenye maambukizi makubwa duniani.
Utafiti unaonesha kuwa idadi ya vifo imeongezeka baada ya maambukizi hayo kuongezeka maradufu katika siku za hivi karibuni katika maeneo ya Dakota Kaskazini na Utah.
Rais Donald Trump ambaye amekuwa akisema kuwa chanjo ya maambukzi hayo itapatikana hivi karibunu, amesema kuwa takwimu zinatisha na kuilaumu tena china kwa misingi kuwa ilishindwa kulidhibiti janga hili mwanzoni.
Trump, aidha ametetea hatua alizopiga kudhibiti janga hilo nchini Marekani, akisema kuwa taifa hilo sasa lingekuwa na zaidi ya vifo milioni mbili asingechukua tahadhari za mapema kinyume na anavyokashifiwa na wapinzani wake.
Hata hivyo mpinzani wake wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu, Joe Biden, amemshtumu rais Trump kwa kushindwa kudhibiti maambukizi hayo.