BRAZIL-CORONA-AFYA

Coronavirus: Kesi zaidi ya 33,500 zathibitishwa nchini Brazil

Katika mtaa wa kibiashara huko Sao Paulo, mji mkuu wa uchumi wa Brazil, nchi ya pili ulimwenguni ambayo inashikilia idadi kubwa zaidi ya watu wenye virusi vya Corona kwa visa zaidi ya milioni 2 nchini.
Katika mtaa wa kibiashara huko Sao Paulo, mji mkuu wa uchumi wa Brazil, nchi ya pili ulimwenguni ambayo inashikilia idadi kubwa zaidi ya watu wenye virusi vya Corona kwa visa zaidi ya milioni 2 nchini. REUTERS/Amanda Perobelli

Brazil imerekodi visa 33,536 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo vipya 836 vinavyohusishwa na janga hilo katika musa wa saa ishirini na nne zilizopita, wizara ya afya imesema.

Matangazo ya kibiashara

Idadi ya visa vya maambukizi nchini Brazili imepindukia zaidi ya milioni 4.59, na jumla ya vifo 138,108 sasa vimerekodiwa, kulingana na takwimu za serikali.

Hayo yanajiri wakati Idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Marekani kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona, sasa imeongezeka na kufikia zaidi ya Laki Mbili, kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.

Pamoja na vifo hivyo, watu wengine Milioni Sita na Laki Nane, wameambukizwa virusi hivyo na kuifanya Marekani kuwa nchi yenye maambukizi makubwa duniani.

Utafiti unaonesha kuwa idadi ya vifo imeongezeka baada ya maambukizi hayo kuongezeka maradufu katika siku za hivi karibuni katika maeneo ya Dakota Kaskazini na Utah.