MAREKANI-CHINA-USHIRIKINAO

Mkutano Mkuu wa UN: Washington na Beijing zarushiana maneneo makali

Donald Trump, hapa akiwa Kenosha, Wisconsin, Septemba 1, 2020.
Donald Trump, hapa akiwa Kenosha, Wisconsin, Septemba 1, 2020. Leah Millis/Reuters

Marekani na china zimeendelea kuonyesha misimamo yao katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa Jumanne wiki hii huko New York, makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano uliofanyika kupitia njia ya video.

Matangazo ya kibiashara

Nchi hizi mbili zimelaumiana kuhusu janga hatari la Corona. Rais wa Marekani Donald Trump ameishambulia Beijing kuhusu hasa suala la janga la Corona na kuilaumu China kwa kueneza virusi vya corona.

Mwenzake wa China, Xi Jinping, amemshtumu mwenzake kwamba ni mbinafsi na ameshindwa kukabiliana vilivyo na ugonjwa huo nchini mwake.

Uhusiano kati ya nchi hizo mbili zenye uwezo umezorota katika nyanja tofauti.

Rais wa Marekani, mara kwa mara, amekuwa akilaumu Beijing kwa kuficha ukweli kuhusu virusi hivyo, akisema wangelisaidia kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa Covid -19. Hata hivyo China imetaja madai hayo kuwa uzushi usiokuwa na msingi wowote.

Kufikia sasa idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Marekani kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona, sasa imeongezeka na kufikia zaidi ya Laki Mbili, kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.

Pamoja na vifo hivyo, watu wengine Milioni Sita na Laki Nane, wameambukizwa virusi hivyo na kuifanya Marekani kuwa nchi yenye maambukizi makubwa duniani.

Utafiti unaonesha kuwa idadi ya vifo imeongezeka baada ya maambukizi hayo kuongezeka maradufu katika siku za hivi karibuni katika maeneo ya Dakota Kaskazini na Utah.

Rais Donald Trump ambaye amekuwa akisema kuwa chanjo ya maambukzi hayo itapatikana hivi karibunu, amesema kuwa takwimu zinatisha na kuilaumu tena china kwa misingi kuwa ilishindwa kulidhibiti janga hili mwanzoni.

Trump, aidha ametetea hatua alizopiga kudhibiti janga hilo nchini Marekani, akisema kuwa taifa hilo sasa lingekuwa na zaidi ya vifo milioni mbili asingechukua tahadhari za mapema kinyume na anavyokashifiwa na wapinzani wake.

Hata hivyo mpinzani wake wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu, Joe Biden, amemshtumu rais Trump kwa kushindwa kudhibiti maambukizi hayo.