BRAZILI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya maambukizi yapindukia milioni 4.6 Brazil

Rais wa Brazili Jair Bolsonaro, Julai 24, 2020.
Rais wa Brazili Jair Bolsonaro, Julai 24, 2020. REUTERS/Adriano Machado

Brazil imerekodi visa vipya 33,281 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo vipya 869 vilivyohusishwa na janga hilo katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, Wizara ya Afya imebaini.

Matangazo ya kibiashara

Kufikia sasa Brazil ina visa milioni 4.6 vya maambukizi, na jumla ya vifo 138,977 vimerekodiwa, kulingana na takwimu za serikali.

Hayo yanajiri wakati Idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Marekani kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona, sasa imeongezeka na kufikia zaidi ya Laki Mbili, kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.

Pamoja na vifo hivyo, watu wengine zaidi ya Milioni Sita na Laki Nane, wameambukizwa virusi hivyo na kuifanya Marekani kuwa nchi yenye maambukizi makubwa duniani.

Utafiti unaonesha kuwa idadi ya vifo imeongezeka baada ya maambukizi hayo kuongezeka maradufu katika siku za hivi karibuni katika maeneo ya Dakota Kaskazini na Utah.