BRAZILI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Tamasha la Rio laahirishwa kutokana na maambukizi zaidi

Brazil ni nchi ya pili kuathirika zaidi na mgogoro wa kiafya baada ya Marekani, kwa suala la maambukizi au vifo.
Brazil ni nchi ya pili kuathirika zaidi na mgogoro wa kiafya baada ya Marekani, kwa suala la maambukizi au vifo. REUTERS

Shule za Samba za Rio de Janeiro nchini Brazil, zimeamua kuahirisha sherehe iliyotarajiwa kufanyika mwezi Februari 2021, wakati nchi hii inaendelea kukabiliana na janga la COVID-19, ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Ligi Huru ya Shule za Samba huko Rio de Janeiro (LIESA) haikutoa tarehe mpya ya sherehe hiyo, ikisema itategemea chanjo dhidi ya virusi ya Corona.

"Ni vigumu kwa kweli kuandaa tamasha bila chanjo," amesema Jorge Castanheira, rais wa LIESA.

Castanheira ameongeza kuwa tamasha hilo linaweza kuahirishwa hadi mwezi Januari 2022 ili lisiingiliane na tamasha linalofuata.

Shule kumi na tatu bora za Samba nchini Brazil zinashiriki mashindano mbele ya zaidi ya wakaazi 90,000, watalii na watu mashuhuri wakati wa sherehe hiyo, ambayo tarehe yake inabadilika kila mwaka kwa sababu inafuatana na kipindi cha mfungo kwa waumini wa Kanisa Katoliki.