MAREKANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Visa vipya 42,340 vya maambukizi vyathibitishwa Marekani

Jimbo la Midwestern limeandikisha rekodi ya visa vipyavya maambukizi ya ugonjwa huo hatari kwa mwezi huu wa Septemba, na California imeendelea kuwa jimbo lililoathiriwa zaidi na visa zaidi ya 800,000 kwa jumla, ikifuatiwa na Texas, Florida na New York.
Jimbo la Midwestern limeandikisha rekodi ya visa vipyavya maambukizi ya ugonjwa huo hatari kwa mwezi huu wa Septemba, na California imeendelea kuwa jimbo lililoathiriwa zaidi na visa zaidi ya 800,000 kwa jumla, ikifuatiwa na Texas, Florida na New York. REUTERS

Vituo vya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa (CDC) nchini Marekani vimeorodhesha visa vipya 42,340 vya maambukizi ya virusi vya Corona siku ya Ijumaa tangu, na kufanya idadi ya maambukizi kufikia 6,958,632 nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

CDC pia imerekodi vifo vipya 918 vilivyotokana na virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa COVID-19, na kufikisha jumla ya vifo 202,329 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Marekani.

Jimbo la Midwestern limeandikisha rekodi ya visa vipyavya maambukizi ya ugonjwa huo hatari kwa mwezi huu wa Septemba, na California imeendelea kuwa jimbo lililoathiriwa zaidi na visa zaidi ya 800,000 kwa jumla, ikifuatiwa na Texas, Florida na New York.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.