Trump kumteua rasmi Amy Coney Barrett kuchukua nafasi ya Jaji RBG
Imechapishwa:
Donald Trump amemteua jaji wa kihafidhina Amy Coney Barrett kuchukua nafasi ya Ruth Bader Ginsburg katika Mahakama Kuu ya Marekani, vyombo vikuu vya habari nchini Marekani vimeripoti, vikunukuu vyanzo kutoka chama cha Republican.
"Tutamtangaza mtu mzuri!", rais wa Marekani amesema ijumaa jioni katika mkutano wa kampeni huko Newport News, katika Jimbo la Virginia, bila hata hivyo kueleza bayana juu ya chaguo lake.
"Nadhani kesho (Jumamosi) itakuwa siku nzuri!", Ameongeza mbele ya umati wa watu waliokuwa wakimshangilia, ambao wamempongeza kwa kutajwa kwa tangazo hilo, ikiwa zimzsalia siku zisizozidi 40 kabla ya uchaguzi urais nchini Marekani.
Rais Donald Trump anatarajia kuthibitisha rasmi Jumamosi saa 5:00 jioni (sawa na 9:00 usiku za za kimataifa) kutoka Ikulu ya White House jina la Amy Coney Barrett, jaji anayejulikana kwa imani yake ya kidini.
Atachukuwa nafasi ya "RBG" ambaye alifariki dunia wiki iliyopita kwa ugonjwa wa saratani.
Kwa Trump hatua hii inampa fursa ya kujiongezea muda katika wakati anapojaribu kuwaimarisha wafuasi wake kabla ya mdahalo unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo na mgombea wa urais kutoka chama cha Democrats Joe Biden.