MAREKANI-USALAMA

Wafuasi wa Breonna Taylor wataka mabadiliko kwenye uongozi wa nchi kupitia kura

Ijumaa jioni, umati wa watu uliandamana kwa amani katika mitaaa ya Louisville, wakiungwa mkono na watu waliokuwa wakiendesha magari, huku wakipiga honi.
Ijumaa jioni, umati wa watu uliandamana kwa amani katika mitaaa ya Louisville, wakiungwa mkono na watu waliokuwa wakiendesha magari, huku wakipiga honi. AFP

"Inatakiwa hatua zichukue nafasi ya maandamano": kwa sauti moja, jamaa za Breonna Taylor, msichana mweusi aliyeuawa na polisi huko Louisville, na wanaharakati wanaopinga ubaguzi wa rangi wameomba kuongeza muda wa maandamano yao ya kihistoria ya hasira katika uchaguzi wa urais nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Kutoka mji huu ambao umekuwa kitovu kipya cha utata kuhusu ukatili wa polisi, wakili Ben Crump, anayejulikana kuwawakilisha wale walio karibu na Breonna Taylor, George Floyd au Jacob Blake, ameomba "mabadiliko ya uongozi" nchini Marekani.

Ijumaa jioni, umati wa watu uliandamana kwa amani katika mitaaa ya Louisville, wakiungwa mkono na watu waliokuwa wakiendesha magari, huku wakipiga honi.

Ikiwa imesalia siku 39 kabla ya uchaguzi wa urais, jiji hili la Kentucky limeendelea kukumbwa na maandamano makubwa. Waandamanaji wameghadhabishwa na kukosekana kwa mashtaka ya mauaji dhidi ya maafisa wa polisi waliomuua Breonna Taylor nyumbani kwake Machi 13.

"Daima watakuwa wao dhidi yetu +," amesema mama yake, Tamika Palmer, kwa maneno yaliyosomwa na dada yake.

Breonna Taylor, 26, alifariki dunia Machi 13, wakati maafisa watatu wa polisi waliingia chumbani kwake baada ya kuvunja mlango usiku wa manane.

Mmoja kati ya maafisa hao watatu wa polisi alishtakiwa, kwa kuhatarisha maisha ya wengine. Hakuna shtaka lililoletwa dhidi ya wenzake wawili, ambao risasi zao zilimuua mfanyakazi mmpja wa hospitali.