MAREKANI-TRUMP-UCHUMI

New York Times: Trump hajalipa kodi za mapato kwa miaka 10

Rais wa Marekani Donald Trump akihutubia hadhira iliyokusanyika kwa mkutano wa chama cha Republican huko Charlotte kutoka Ikulu ya White House, Agosti 27, 2020.
Rais wa Marekani Donald Trump akihutubia hadhira iliyokusanyika kwa mkutano wa chama cha Republican huko Charlotte kutoka Ikulu ya White House, Agosti 27, 2020. AP/Evan Vucci

Rais wa Marekani Donald Trump anadaiwa kuwa ahajalipa kodi za mapato kwa miaka 10. Kulingana na gazeti la New York Times, raia Donald trump alilipa tu dola 750 ya kodi mwaka alipochaguliwa.

Matangazo ya kibiashara

Suala hili limeendelea kuzua gumzo nchini Marekani kwa miaka minne sasa.

New York Times imebaini kwamba maneno ya Donald Trump yako mbali na ukweli. Gazeti hili la kila siku linasema limefaulu kupata taarifa za mapato ya kodi ya tajiri huyo zamani wa mali isiyohamishika kwa zaidi ya miaka ishirini na limehakikisha kuwa kati ya makampuni zaidi ya mia moja zinazomilikiwa na rais Donald Trump, mengi yanakabiliwa na matatizo.

Inadaiwa kuwa kila mwaka, Donald Trump anakumbwa na hasara zaidi kuliko faida. Na ni kwa sababu hiyo alilipa tu dola 750 mwaka 2016 na dola 750 mwaka 2017. Na kabla ya kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi, hajalipa chochote kwa miaka kumi. Kulingana na Gazeti la New York Times, kati ya makampuni 100 yanayomilikiwa na Donald Trump, mengi yamekumbwa na hasara kubwa.

Kwa upande wake rais Donald Trump amefutilia mbali tuhuma hizo dhidi yake: "Nililipa sana, na nililipa kodi nyingi ya mapato katika ngazi ya serikali pia! Jimbo la New York linatoza kodi kubwa! Zote hizi ni habari za uzushi. Gazeti la New York Times linajaribu tu kuzua… linajaribu kufanya linaloweza! "

Trump anajitayarisha kwa mdahalo wa ana kwa ana unaofanyika Jumanne wiki hii, kati yake na mgombea wa chama cha Democratic, Joe Biden.