MAREKANI-MDAHALO-SIASA

Donald Trump na Joe Biden washambuliana katika mdahalo

Wagombea wa urais Donald Trump na Joe Biden walitafautiana takribani kwenye kila swali walilorushiwa na mwenyekiti wa mdahalo huo: kuanzia masuala ya afya, usalama, hadi ya kifamilia, Cleveland (Ohio) Jumanne, Septemba 29, 2020.
Wagombea wa urais Donald Trump na Joe Biden walitafautiana takribani kwenye kila swali walilorushiwa na mwenyekiti wa mdahalo huo: kuanzia masuala ya afya, usalama, hadi ya kifamilia, Cleveland (Ohio) Jumanne, Septemba 29, 2020. REUTERS/Brian Snyder

Mdahalo kati ya wagombea wawili katika uchaguzi wa urais wa Marekani umefanyika katika hali ya mvutano na matusi, huku kila mmoja akimshtumu mwengine.

Matangazo ya kibiashara

Wawili hawa walitafautiana takribani kwenye kila swali walilorushiwa na mwenyekiti wa mdahalo huo: kuanzia masuala ya afya, usalama, hadi ya kifamilia.

Mdahalo huo ulifuatwa na mamilioni ya watu, hasa Wamarekani ambao wengi walitarajia kuwa wagombea hao wawili watazungumzia masuali nyeti yanayotakiwa kupewa kipaumbelea katika nchi hiyo inayoendelea kuzongwa na ugonjwa hatari wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya Corona.

Mdahalo huo umefanywa kwa msururu wa kurushiana vijembe , ambavyo ni pamoja na Trump kuhoji ujasusi wa Biden na Biden akimwita Trump kichekesho, akimnyamazisha, kwa hasira, "Je! Utanyamaza, jamani?"

Mdahalo huo uliendeshwa na Chris Wallace, mwandishi wa kituo cha televisheni cha Fox News.

Mdahalo huo uligubikwa na masuala kuhusu janga la COVID-19, Mahakama Kuu, uchumi, ubaguzi wa rangi na machafuko yaliyokumba baadhi ya mijini, sera za kila mmoja wa wagombea na 'ukweli wa matokeo ya uchaguzi'.

■ Mahakama Kuu

Swali la kwanza lilihusiana na uteuzi wa Jaji mpya wa Mahakama Kuu, Amy Coney Barrett, siku chache zilizopita. "Atakuwa wa kipekee na mwenye nguvu kuliko watangulizi wake," ameahidi Donald Trump, ambaye alipewa nafasi ya kwanza ya kujibu.

"Tunafikiria sio sahihi" kuteua mtu kama huyo katika zikisalia siku chache kabla ya uchaguzi, amejibu Joe Biden, "tunapaswa kusubiri kuona matokeo ya uchaguzi huu", ameongeza mgombea wa chama cha Democratic. "Tulishinda uchaguzi" wa 2016 "na tuna haki ya kufanya hivyo," amejibu rais anayemaliza muda wake Donald Trump.