MAREKANI-TRUMP-CORONA-AFYA

Coronavirus: Donald Trump alazwa hospitali 'kwa siku chache'

Mgombea urais wa chama cha Democratic nchini Marekani Joe Biden ambaye alipimwa na hakupatikana na virusi vya Corona alianza tena kampeni yake Ijumaa, Oktoba 2, wakati Donald Trump, ambaye alipatikana na virusi hivyo, atalazimika kulazwa hospitali kwa siku chache.

Rais Donald Trump atatibiwa katika Hospitali ya Walter Reed katika jiji la Washington.
Rais Donald Trump atatibiwa katika Hospitali ya Walter Reed katika jiji la Washington. AP Photo/J. Scott Applewhite
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani amepelekwa hospitali kwa siku chache kwa mapendekezo ya madaktari. Kulingana na taarifa kutoka Ikulu ya White House, hii ni hatua ya tahadhari na Donald Trump atakuwa akifanya kazi kutoka hospitali ya Walter Reed katika viunga vya Washington.

Mkewe Melania Trump, ambaye pia ameathiriwa na janga hilo, anaugua kikohozi kidogo na maumivu ya kichwa.

Kiongozi wa wengi kutoka chama cha Democratic katika Baraza la Wawakilishi, Nancy Pelosi, amemtakia afueni rais Donald Trump baada ya taarifa kuwa alipatikana na ugonjwa wa Covid-19. "mapema jana asubuhi.

Kwa upande wake, rais wa zamani wa Marekani Barack Obama alisema siku ya Ijumaa "tunataka pia kumtakia kila la heri rais wa Marekani [na] mkewe rais", pia alizungumza kwa niaba ya mkewe Michelle Obama. Pia alibaini "mapambano makubwa ya kisiasa" kati ya Wademocrats na Warepublican.

Inasemekana kwamba Trump mwenye umri wa miaka 74, anasumbuliwa na homa na kwamba atapewa dawa ambayo bado inafanyiwa majaribio.

Rais huyo wa Marekani wa chama cha Republican amepata ugonjwa wa COVID-19 akiwa katikati ya kampeni kuelekea uchaguzi wa mwezi Novemba ambapo atachuana na mpinzani wake wa chama cha Democratic Joe Biden.