Madaktari: Trump anaweza kuondoka hospitalini Jumatatu
Imechapishwa:
Rais wa Marekani Donald Trump bado yupo hospitalini kwa kuangalizi wa karibu baada ya kuambukizwa virusi vya Corona wiki iliyopita pamoja na mke wake.
Wakati huu maswali mengi yakiulizwa kuhusu hali ya afya yake, Madaktari wake wanasema anaendelea vizuri na huenda akaruhusiwa kuondoka hospitalini siku ya Jumatatu, baada ya kuongezewa hewa mara mbili.
Siku ya Jumapili, rais Trump alionekana nje ya hospitali akiwa ndani ya gari akiwa amevalia barakoa, akiwapungua mkono wafuasi wake, hatua ambayo imelaaniwa na baadhi ya watu wanaosema ni hatari kwa afya za watu aliokaribiana nao.
Rais Trump ni miongoni mwa Wamarekani zaidi ya Milioni Saba ambao wameambukizwa virusi vya Corona, huku wengine zaidi ya Laki Mbili wakipoteza maisha.