MAREKANI-CORONA-AFYA

Wafanyakazi kadhaa wa White House waambukizwa virusi vya Corona Marekani

Baadhi ya wafanyakazi wa hivi punde kuambukizwa ni pamoja na, mshauri mkuu katika ikulu ya White House, Stephen Miller, ambaye amekuwa karantini kwa siku chache zilizopita, na afisa mkuu katika jeshi.
Baadhi ya wafanyakazi wa hivi punde kuambukizwa ni pamoja na, mshauri mkuu katika ikulu ya White House, Stephen Miller, ambaye amekuwa karantini kwa siku chache zilizopita, na afisa mkuu katika jeshi. REUTERS/Joshua Roberts

Wafanyakazi zaidi katika ikulu ya Marekani wamepatikana na viruisi vya corona, siku chache tu baada ya rais Donald Trump kulazwa hospitalini baada ya kupatikana na virusi hivyo.

Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya wafanyakazi wa hivi punde kuambukizwa ni pamoja na, mshauri mkuu katika ikulu ya White House, Stephen Miller, ambaye amekuwa karantini kwa siku chache zilizopita, na afisa mkuu katika jeshi.

Aidha, kwa sasa, Jenerali wa juu wa Marekani Mark Milley na viongozi wengine wa kijeshi wamejitenga baada ya Charles Ray kupatikana na maambukizi hayo.

Hayo yakijiri, kati ya maafisa waliohudhuria mikutano na Charles Ray juma lililopita ambao kwa sasa wako karantini, hakuna mmoja wao ambaye amethibitika kuwa na maambukizi hayo au hata kuonesha dalili zozote za ugonjwa huo

Wengine ambao wameambukizwa ni pamoja na mke wa rais Trump Melania Trump, mshirika wa karibu wa Trump, Hope Hicks na baadhi ya maseneta wa chama cha Republican.