BRAZILI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya maambukizi yapindukia zaidi ya Milioni 5 Brazil

Rais Jair Bolsonaro amekuwa akikashifiwa kwa kukosa kutilia maanani vita dhidi ya Corona.
Rais Jair Bolsonaro amekuwa akikashifiwa kwa kukosa kutilia maanani vita dhidi ya Corona. REUTERS/Adriano Machado TPX IMAGES OF THE DAY

Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona nchini Brazil imepita watu milioni tano wakati ambapo idadi ya watu waliofariki kutokana na athari za janga hilo ikifikia watu laki moja na hamsini ,imesema mamlaka nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Brazili ni taifa la tatu duniani ambalo lina maambukizi mengi ya virusi vya Corona baada ya Marekani na india, hali ambayo inajiri baada ya rais Jair Bolsonaro kukashifiwa kwa kukosa kutilia maanani vita dhidi ya Corona.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.