MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA

Kamala Harris na Mike Pence wapambana katika mdahalo wa televisheni

Kamala Harris, Seneta na mgombea mwenza wa Joe Biden, anapambana katika mdahalo na Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence Oktoba 7, 2020 huko Salt Lake City, Utah.
Kamala Harris, Seneta na mgombea mwenza wa Joe Biden, anapambana katika mdahalo na Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence Oktoba 7, 2020 huko Salt Lake City, Utah. AFP Photos/Morry Gash

Nchini Marekani kuelekea Uchaguzi wa urais tarehe tatu mwezi Novemba, Kamala Harris anayewanianafasi ya makamu wa rais kupitia chama cha Democratic, amekuwa akichuana na Mike Pence wa Republican katika mdahalo wa Televisheni, kutafuta uungwaji mkono, wakigusia masuala mbalimbali yanayolikumba taifa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Kinyume na mdahalo wa kwanza kati ya wagombea urais Joe Biden na Donald Trump uliotawaliwa na majibizano makali wiki iliyopita, Kamala na Pence walionekana watulivu.

Bi. Harris ametumia mdahalo huu kuushtumu utawala wa Trump kwa kushindwa kukabiliana na janga la Corona ambalo limewaambukiza watu zaidi ya Milioni Saba nchini humo.

Hata hivyo, Pence,61, amekanusha madai hayo na kusema utawala wake na Trump umefanya vya kutosha kukabiliana na janga hilo na kuongeza kuwa wapinzani wao wanatia siasa katika makabiliano dhidi ya janga hili.

Mdahalo huu uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Utah, umetangulia Mdahalo mwingine kati ya Trump na Biden hivi karibuni, kuendelea kuwaomba Wamarekani kuwapigia kura.

Uchaguzi wa urais wa Marekani umepangwa kufanyikja Novemba 3, 2020.