MAREKANI-TRUMP-CORONA-AFYA

Donald Trump aruhusiwa kufanya shughuli zake za kawaida

Ripoti kutoka Ikulu ya White House, inaeleza kuwa Daktari huyo ameeleza kuwa, kwa sasa rais Trump haoneshi dalili zozote za maambukizi hayo.
Ripoti kutoka Ikulu ya White House, inaeleza kuwa Daktari huyo ameeleza kuwa, kwa sasa rais Trump haoneshi dalili zozote za maambukizi hayo. MANDEL NGAN / AFP

Daktari wa rais wa Marekani Donald Trump anasema kiongozi huyo amemaliza matibabu yake dhidi ya virusi vya Corona na sasa anaweza kurejea katika shughuli zake za kawaida kuanzia mwishoni mwa wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Daktari Sean Conley amesema rais Trump amekuwa akipata nafuu haraka na sasa yupo katika hali nzuri na imara ya kiafya.

Ripoti kutoka Ikulu ya White House, inaeleza kuwa Daktari huyo ameeleza kuwa, kwa sasa rais Trump haoneshi dalili zozote za maambukizi hayo.

Jumamosi itakuwa ni siku 10 tangu Trump alipoanza kupokea matibabu katika kipindi ambacho alishuhudiwa akilazwa hospitalini na baadaye kuruhusiwa.

Katika hatua nyingine, Trump amejiondoa katika mdahalo wa pili dhidi ya mpinzani wake Joe Biden Alhamisi ijayo, baada ya waandalizi kupendekeza kuwa ufanyike kwa njia ya vídeo.

Biden yeye amesisitiza kuwa atashiriki katika mdahalo huo mwenyewe hata bila ya rais Trump.

Hadi sasa haijafahamika iwapo mdahalo huo utafanyika, huku wa mwisho ukipangwa kufanyika tarehe 22 mwezo huu, lakini haijafahamika utafanyika kwa njia gani.

Uchaguzi wa urais nchini Marekani umepangwa kufanyika tarehe tatu mwezi Novemba.