BRAZILI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Brazil yakaribia kufikisha vifo 150,000

Brazil ni taifa la tatu duniani ambalo lina maambukizi mengi ya virusi vya Corona baada ya Marekani na india, hali ambayo inajiri baada ya rais Jair Bolsonaro kukashifiwa kwa kukosa kutilia maanani vita dhidi ya Corona.
Brazil ni taifa la tatu duniani ambalo lina maambukizi mengi ya virusi vya Corona baada ya Marekani na india, hali ambayo inajiri baada ya rais Jair Bolsonaro kukashifiwa kwa kukosa kutilia maanani vita dhidi ya Corona. REUTERS

Karibu watu 150,000 wamekufa kutokana na Covid-19 nchini Brazil, moja ya nchi zilizoathirika zaidi duniani na janga la Corona, kulingana na takwimu za hivi karibuni zilizotolewa Ijumaa na maafisa wa afya.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Afya nchini Brazili imeripoti vifo vipya 682 katika muda wa saa 24 zilizopita, na kufikisha jumla ya vifo 149,639 tangu kuzuka kwa janga hilo.

Brazil imerekodi visa vipya 27,444 vya maambukizi ya virusi vya Corona, na kufikisha jumla ya visa 5,055,888.

Brazil ni taifa la tatu duniani ambalo lina maambukizi mengi ya virusi vya Corona baada ya Marekani na india, hali ambayo inajiri baada ya rais Jair Bolsonaro kukashifiwa kwa kukosa kutilia maanani vita dhidi ya Corona.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.