Trump afanya kampeni yake ya kwanza Florida baada ya kupona Corona
Imechapishwa:
Baada ya kukatiza kampeni yake kwa sababu ya kuambukizwa virusi vya Corona, rais wa Marekani amerejelea tena kampeni za kusaka urais kuelekea Uchaguzi Mkuu Novemba 3, baada ya kusema amepona maambukizi hayo.
Trump amewahotubua wafuasi wake katika majimbo ya Florida, Pennsylvania na Iowa maeneo ambayo ni muhimu sana kwake kuelekea katika kinyang'anyiro dhidi ya Joe Biden wa chama cha Democratic.
Awali Trump aliendelea kusisitiza kuwa, nchi yake inakaribia kupata chanjo dhidi ya virusi vya Corona.
Katika hatua nyingine, Kamati ya Senate imeanza kusikiliza pendekezio la rais Trump, kuwa Amy Coney Barrett awe mmoja wa Majaji katika Mahakama ya Juu.
Kulingana na uchunguzi kuhusu uchaguzi huo, Trump amepoteza wafuasi wengi. Ili kushinda, lazima apanue wigo wake wa uchaguzi. Lakini rais anaendelea kusema: mnamo mwaka 2016, hakuna mtu aliyetabiri ushindi wake. Na ametangaza kwamba atapa ushindi mkubwa ambao utawashangaza wengi mwezi Novemba.