MAREKANI-OBAMA-SIASA-USALAMA

Obama kufanya kampeni kwa niaba ya Biden, siku moja kabla ya mdahalo wa mwisho

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama wakati wa mkutano kwa njia ya video, Juni 3, 2020.
Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama wakati wa mkutano kwa njia ya video, Juni 3, 2020. THE OBAMA FOUNDATION / AFP

Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama, ambaye alikuwa hajajitokeza hadharani kwa miaka kadhaa, atafanya mkutano wake wa kwanza wa kampeni kwa niaba ya Joe Biden leo Jumatano, wakati makamu wake wa zamani wa rais yuko kwenye kinyang'anyiro kikali na Donald Trump siku 13 kabla ya uchaguzi wa rais wa Novemba 3.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa zamani wa Marekani atajikita hasa kwa kuhamasisha upigaji kura wa mapema kwa niaba ya mgombea wa chama cha Democratic katika mkutano wa hadhara huko Philadelphia, jiji kuu la Pennsylvania, moja wapo ya majimbo muhimu kwa uchaguzi, chanzo kilicho karibu na Obama kimesema.

Donald Trump, ambaye alikuwa huko Pennsylvania Jumanne usiku, atakuwa North Carolina, jimbo lingine muhimu ambapo yeye na mpizani wakeJoe Biden wanakaribiana kwa kura, kulingana na uchunguzi.

Hatua ya Barack Obama kumuunga mkono hadharani Joe Biden, inakuja inakuja wakati muhimu wa kampeni.

Kuingilia kati kwa Barack Obama kutajaza pengo kwa upande wa chama cha Democrat, kwa sababu Joe Biden amesitisha kampeni yake tangu Jumatatu na amejifungia na washauri wake katika nyumba yake ya Delaware ili kujiandaa kwa mjadala wa Alhamisi.