MAREKANI-SIASA-USALAMA

Uchaguzi Marekani: Barack Obama katika kampeni amshambulia Donald Trump

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama katika kampeni kwa niaba ya  wa mgombea wa  chama cha Democratic Joe Biden, Oktoba 21, 2020 huko Philadelphia.
Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama katika kampeni kwa niaba ya wa mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden, Oktoba 21, 2020 huko Philadelphia. AP Photo/ Matt Slocum

Rais wa zamani aw Marekani Barack Obama amefanya kampeni yake ya kwanza kumpigia debe Joe Biden anayepeperusha bendera ya chama cha Democratic katika kinyang'anyiro cha urais nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Rais huyo wa zamani wa Marekani ametoa hotuba kali kwa wafuasi wa chama cha Democratic ambao walilazimika kusalia ndani ya magari yao kutokana na janga la COVID-19.

Wakati huo huo alimshambuliwa kwa maneno makali rais anaye maliza muda wake Donald Trump, ambaye anawania kwa muhula mwingine katika uchaguzi huo uliopangwa rasmi kufanyika Novemba 3.

"Ninaelewa rais huyu anataka apongezwe kwa uchumi aliorithi na hataki kukosolewa kwa janga alilopuuzia. Lakini mnajua, hakutakiwa afanye hivyo. Kuandika ujumbe kwenye ukurasa wako wa Twitter mbele ya televisheni yako haitatui matatizo. Kusema habari zisizokuwa na msingi hakuboreshi maisha ya watu, " amesema Barack Obama akimshambuliwa rais Trump.

Zikiwa zimebaki wiki mbili tu kabla ya uchaguzi huo, tofauti ya mikakati ya kampeni za wagombea hao ipo wazi.

Mgombea wa chama cha Republican Donald Trump mwenye umri wa miaka 74, aliongoza mkutano mwingine wa kampeni katika jimbo muhimu la Pennsylvania, wakati mpinzani wake wa chama cha Democratic Joe Biden mwenye umri wa miaka 77, akiamuwa kubakia nyumbani Delaware ambako alijiweka karantini kabla ya mdahalo muhimu wa televisheni kati ya wagombea hao wawili leo Alhamisi.

Utafiti wa maoni unaonyesha kuwa Biden anaongoza dhidi ya Trump.